TARATIBU ZA KISHERIA ZA UANZISHAJI WA BIASHARA
- Details
- Category: Uchumi na Biashara
- Published on Tuesday, 12 January 2016 13:34
- Written by Jonathan Mwanshinga
- Hits: 4101
Kupitia
ukurasa huu, napenda kuufahamisha umma, hasa kwa wale wenye njozi ya
kuanzisha biashara mpya kwenye ardhi ya Tanzania. Yaweza kuwa mojawapo
kati ya biashara zifuatazo, yaani biashara ya mtu binafsi (sole
proprietorship), biashara ya Ubia (partnership) na biashara za
makampuni.
MMILIKI BINAFSI (SOLE PROPRIETORSHIP)
Kwa wamiliki binafsi wa biashara wazawa au wageni wanahitaji kuwa na vitu vifuatavyo:
- TIN
- Leseni ya biashara
-Akaunti katika benki ya biashara
Kwa mtu ambaye sio raia wa Tanzania anapaswa kuwa na kibali
kinachomruhusu kufanya biashara nchini kutoka Idara ya Uhamiaji.
TIN ni kifupisho cha maneno Taxpayer Identification Number, kwa
Kiswahili namba ya utambulisho wa mlipa kodi. Ni muhimu kwa
mfanyibiashara yeyote kusajiliwa na kutambulika kama mlipa kodi kupitia
mamlaka ya mapato Tanzania kwani TIN ni kama uthibitisho wa
mfanyabiashara kutambuliwa na mamlaka na taasisi yoyote ya kibiashara
kama vile mamlaka za miji zinazotoa vibali vya biashara pamoja na
mamlaka ya mapato yenyewe. Huwezi kufanya biashara na taasisi kubwa kama
vile kupewa uzabuni wa kusambaza bidhaa bila kuwa na TIN.
Baadhi
ya makampuni ya mawasiliano hutoa wakala kwa watu binafsi kutoa huduma
za kutuma na kupokea fedha kupitia mitandao ya simu kama vile M-PESA,
TIGO PESA, AIR TEL MONEY na mitandao mingine mingi. Moja ya vigezo
vikubwa vya kupewa wakala wa mitandoa hii ni kuwa na TIN. Baadhi ya
wafanyabiashara wanaochukua uwakala wa kampuni za simu ama kwa kufahamu
au kwa kutofahamu wameunganishwa na wakala mwingine katikati na
kuwafanya wao kuwa watu wa tatu. Hii inapunguza kamisheni ambayo wakala
anapata kwa kuwa kuna sehemu ya malipo inayokwenda kwa huyu mtu wa kati.
TIN
inatolewa bure na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), hakuna usumbufu
katika upatikanaji wa TIN. TIN inaweza kupatikana ndani ya siku 1 hadi 2
kutegemeana na idadi ya maombi ambayo mamlaka imepokea kwa kipindi
husika. Mlipa kodi ni lazima afike TRA ili kujiandikisha kupitia
biometric scanning inayohusisha kuchukuliwa picha, alama za vidole na
sahihi.
Katika
kukamilisha zoezi hili ni vema muhusika akafika moja kwa moja TRA. Siku
hizi kwa ajili ya kugawana ridhiki, wapo watu wa kati wengi ambao
husaidia kuwaunganisha waombaji wa TIN na TRA. Watu hawa hutumia ushamba
wa watu wengi kujipatia sehemu ya kipato. Si mbaya sana kuwa nao lakini
baadhi yao huwatoza wateja wao ujira mkubwa ambao hufanya zoezi la
kuomba TIN kuwa na gharama kubwa wakati inaelezwa na mamlaka husika kuwa
ni bure. Hata kama muombaji wa TIN atamtumia mtu wa kati ni muhimu
yeyemwenyewe kuwepo ili kutoa ushirikiano atakapotakiwa kuchukuliwa
picha na sahihi.
Lakini
pia kufika TRA kwa mfanyabiashara mpya ni muhimu ili kuweza kupata
maelezo ya ziada yanahusiana na biashara mpya na msaada wa kitaalamu.
Mfanyabiashara atapata fursa ya kuwauliza maafisa wa TRA maswali kadhaa
kuhusu biashara kama vile ni kwa nini vipo vyombo vingine vinavyoweza
kukamata au kuzuia mzigo unaposafirishwa kutoka duka la jumla, na nini
afanye ili kuepukana na usumbufu kama huu? Ni kazi ya maafisa wa TRA
kukujibu maswali yote hayo bila malipo kwani ni moja ya kazi
walizoajiriwa kuzifanya.
Kwa
kujisajili kupata namba ya mlipa kodi inaonesha kuwa unatambua wajibu
wako kama mfanyabiashara wa kuchangia pato la taifa kwa njia ya kulipa
kodi. Na jambo hili ni jema tu kama alivyowahi kusema Arthur Vanderbilt "Taxes
are the lifeblood of government and no taxpayer should be permitted to
escape the payment of his just share of the burden of contributing
thereto." Na Richard M. Nixonaliyesema “Make sure you pay your taxes; otherwise you can get in a lot of trouble.”
LESENI YA BIASHARA
Unatakiwa
kuwa na leseni ya biashara ambayo hupatikana katika ofisi za manispaa
husika chini ya Sheria ya Leseni ya Biashara Sura ya 208 kifungu cha 3
ambacho kinasema ni marufuku kufanya biashara bila kuwa na leseni halali
katika eneo halali.
Muombaji
wa leseni anatakiwa kufika katika moja ya ofisi ya afisa biashara
katika wilaya au manispaa au mji au katika ofisi za wizara ambao ndio
wanahusika na utoaji wa vibali vya biashara katika maeneo husika.
Mtu
yeyote raia wa Tanzania anayo haki ya kupatiwa leseni ya biashara ili
mradi awe ametimiza umri wa miaka kumi na nane (18) mwenye akili timamu
ambaye hajawahi kupatikana na kosa la jinai na awe na eneo la kufanyia
biashara linalokubalika kisheria. Kwa mtu ambaye sio raia wa Tanzania
anapaswa kuwa na kibali kinachomruhusu kufanya biashara nchini kutoka
Idara ya Uhamiaji.
Baada
ya kujaza fomu na viambatanisho, maombi hupitishwa ngazi zinazotakiwa
kisheria – Mpango Miji na Afya. Baada ya hapo leseni hutolewa ndani ya
siku moja au mbili na si zaidi.
Acaunti ya benki itamuwezesha mfanyabiashara kuhifadhi na kupokea fedha kama malipo dhidi ya washirika wake kibiashara.
2. BIASHARA YA UBIA (PARTNERSHIP)
Kwa
watu wanaotaka kufanya biashara kwa kuingia ubia ni lazima wafanye
kwanza usajili kwa msajili wa makampuni BRELA na kupewa cheti cha
umiliki kinachoonesha idadi na majina ya wabia katika biashara husika na
asilimia za uchangiaji katika biashara.
Katika kuomba TIN wabia watatakiwa kuwasilisha nakala ya cheti cha usajili toka BRELA.
Kila mwanachama katika biashara ya ubia atatakiwa kuomba TIN, ikiwa mmoja wao alikuwa nayo hatatakiwa kuomba tena.
3. MIFUKO YA DHAMANA
Mwenye
dhamana anatakiwa kuomba usajili BRELA kwanza na kupewa cheti cha
usajili kinachoonesha majina na anuani za wenye dhamana . Na pia kila
mwanachama anatakiwa kuwa na TIN.
4. MASHIRIKA YA UTU
Taasisi
hizi ni lazima zipate ukubali wa kujiendesha kutoka kwa kamishina.
Maombi ni vema yakaambatanishwa na nyaraka ambatanishi kutoka wizara ya
mambo ya ndani.
5. KAMPUNI
Uanzishaji
wa kampuni unahitaji kusajili jina la biashara kwa Wakala wa Usajili wa
Biashara (BRERA; Business Regulatory and License Agency).
Promota wa kampuni anatakiwa kuwasilisha kwa msajili kanuni za uendeshaji wa kampuni (memorandum and articles of association).
Cheti
cha ushiriki katika biashara toka BRELA kitaambatanishwa wakati wa
kufanya maombi ya TIN pamoja na kanuni za uendeshaji wa biashara.
UTARATIBU WA KUPATA LESENI YA BIASHARA
Mwombaji anapaswa kujaza fomu ya maombi 9TFN kikamilifu na kuambatanisha kivuli cha:-
(i) Jina la Biashara kama sio mtu binafsi (Certificate of Incorporation or Registration).
(ii) “Memorandum and Article of Association” kama ni Kampuni
(iii) Kitambulisho
cha mpiga kura, Cheti cha kuzaliwa au Hati ya kiapo kuonyesha kuwa ni
Mtanzania na Mgeni Hati ya kuishi nchini daraja la “A” (Residnece Permit
Class “A”).
(iv) Hati ya kiuwakili (prowess of a Honey) kama wenye hisa wote wa Kampuni wapo nje ya nchi.
(v) Ushahidi
wa maandishi kuwa ana mahali pa, kufanyia biashara (Kwa mfano hati za
nyumba, mkataba wa upangishaji, risiti za malipo ya kodi za majengo au
ardhi.
(vi) Hati ya kujiandikisha kama mlipa kodi TRA (TIN).
Kwa
leseni zinazodhibitiwa na Mamlaka mbalimbali , Kwa mfano (TFDA, EWURA,
TAURA, CRB, TILLI) n.k lazima mwomaji kuwa na leseni husika kabla ya
kuomba leseni ya biashara.
Leseni
hizi hutolewa kulingana na shughuli unayotaka kuifanya, kwa mfano kuna
biashara zinalazimisha uwe na leseni kutoka Shirika la Viwango la Taifa
(TBS), TFDA, Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Baraza la
Wakala wa Usalama na Afya mahala pakazi (OSHA) na nyinginezo.
Utaratibu wa wajasiriamali wadogo na wa kati (smes) kuwezeshwa kupata alama ya ubora ya ‘tbs’
Serikali
hutenga fedha kila mwaka kwa ajili ya kuhudumia wajasiriamali wadogo na
wa kati pale wanapoomba bidhaa zao wanazozizalisha wenyewe
zithibitishwe ubora. Katika utaratibu huu, wapo wajasiriamali ambao
husamehewa kulipa ada yoyote kwa sababu ya mitaji yao kuwa midogo.
Ili kupata msamaha huu, vigezo vifuatavyo huzingatiwa:
Mjasiriamali
hutakiwa kuwa na barua ya utambulisho kutoka ofisi ya SIDO iliyo
karibu. Ni vema kuhakikisha kuwa barua inafafanua vizuri na kwa kina
shughuli zinazofanywa.
Kwa wale wanaozalisha vyakula huhitajika kuwa na taarifa fupi kutoka Idara ya Afya iliyo karibu na mahali pa uzalishaji au cheti cha TFDA.
Kwa wale wanaozalisha vyakula huhitajika kuwa na taarifa fupi kutoka Idara ya Afya iliyo karibu na mahali pa uzalishaji au cheti cha TFDA.
Mjasiriamali hupaswa kuwa na leseni ya biashara.
Wajasiriamali
waliokwishapata leseni ya kutumia alama ya ubora hupaswa kutunza rekodi
za uzalishaji na mauzo ambazo watatakiwa kuzionesha kwa wakaguzi wa TBS
pindi zinapohitajika.
HATUA ZA KUPATA ALAMA YA UBORA YA ‘tbs’
1. HATUA YA KWANZA – MAOMBI
Maombi ya uthibitishaji wa ubora wa bidhaa hufanywa na mwombaji kwenda kwa Mkurugenzi Mkuu wa TBS kwa maandishi.
Majibu hutolewa yakielezea taratibu na gharama zote.
Majibu huambatana na fomu maalum ambayo mwombaji huijaza na kuirudisha TBS ikiwa na viambatanisho vifuatavyo:
Mtiririko wa uzalishaji wa bidhaa husika;
Mfumo wa uongozi ukionyesha kitengo cha udhibiti ubora;
Orodha ya malighafi anazotumia na mahali zinakotoka kwa kila bidhaa;
Ramani inayoelekeza jinsi ya kufika kiwandani kwako;
Baada ya hapo tarehe ya kufanya ukaguzi wa awali hupangwa.
2. HATUA YA PILI – UKAGUZI WA AWALI
Ukaguzi wa awali hufanywa na wakaguzi wa TBS wakati kiwanda kikiwa katika uzalishaji.
Sampuli huchukuliwa na kupimwa ili kuona kama zinakidhi matakwa ya kiwango husika.
Mkaguzi huandaa taarifa kuhusu hali halisi ya kiwanda na mambo yanayostahili kurekebishwa.
Mkaguzi huandaa taarifa kuhusu hali halisi ya kiwanda na mambo yanayostahili kurekebishwa.
3. HATUA YA TATU – UPIMAJI
Sampuli zilizochukuliwa hupimwa katika maabara za TBS kwa kufuata kiwango husika.
Baada ya kazi ya upimaji kumalizika, ripoti ya maabara hutolewa kwa mwombaji.
4. HATUA YA NNE – UTOAJI WA LESENI
Maamuzi
kuhusu kutoa au kutotoa leseni ya kutumia alama ya ubora hutegemea tu
ripoti ya ukaguzi wa awali wa kiwanda pamoja na ripoti ya maabara.
Kimsingi
ripoti zote mbili zinatakiwa kuonyesha kwamba mazingira ya uzalishaji
kiwandani, mfumo wa uzalishaji na bidhaa iliyopimwa havina matatizo.
Ikiwa sivyo basi mzalishaji hutakiwa kufanya marekebisho na baadaye mkaguzi wa TBS hutumwa tena na kuleta sampuli nyingine.
MUDA WA LESENI (VALIDITY OF LICENCE) YA ALAMA YA UBORA YA ‘tbs’
Leseni
ya kutumia alama ya ubora ya ‘tbs’ hudumu kwa mwaka mmoja na huhuishwa
(renewal) baada ya kuhakikisha kwamba taratibu zilizokubalika (Scheme of
Inspection and Test, SIT) zinafuatwa.
Biashara
za sekta ndogo zinazojihusisha na uvunaji maliasili kama vile uchimbaji
madini na madini ya ujenzi (mawe, kokoto, mchanga); uvuvi; kuni na
uchomaji mkaa, hazihitaji kusajiliwa na BRELA, bali vibali na leseni
zake hutolewa na sekta husika.
b. Biashara katika sekta ndogo nyingine zote zinahitaji kusajiliwa na BRELA, yenye ofisi zake jijini Dar es Salaam.
c.
Kuna kundi la tatu la biashara, ambazo haziko rasmi, na hizi husajiliwa
kwa kupewa leseni ya Nguvu Kazi. Leseni za Nguvu Kazi hutolewa na
mamlaka za serikali za mitaa chini ya Sheria ya Maendeleo ya Rasilimali
Watu, kwa lengo la kuzitambua biashara ndogo ndogo. Idara ya Maendeleo
ya Jamii na Idara ya Maendeleo ya Ushirika katika ngazi ya halmashauri
zinahusika tu katika kusajili vikundi vya wakulima na wafanyabiashara
katika maeneo yao. Kampuni zote sharti zisajiliwe na Wakala wa Usajili
wa Biashara na Leseni (BRELA) au mamlaka nyingine inayoruhusiwa
kisheria.
LESENI ZA VILEO
Sheria ya leseni za vileo imenyambulisha aina tisa za leseni za vileo zinazoweza kutolewa chini ya sheria hii:
Retailers On
Leseni hii humruhusu mwenye biashara kuuza pombe na kunywa eneo la biashara
RETAILERS OFF
Leseni
hii haimruhusu mtu kinywea pombe eneo la biashara bali kwa watu
wanaochukua kunyewea majumbani (Take away) kama Groceries.
WHOLESALE Leseni hii ni kuuza pombe kwa jumla
HOTEL
Leseni hii humruhusu mwenye leseni kuuza pombe kwa ajili ya kunywea
katika eneo la biashara kwa watu waliopanga hotelini kwa wakati wowote
wa mchana na usiku
RESTAURANT
Leseni hii inamruhusu mwenye leseni kuuza pombe kwa mtu yeyote
anayekula chakula katika mgahawa katika muda wa saa 6.00 mchana hadi saa
8.00 mchana na saa 12.00 hadi saa 6.00 usiku.
MEMBERS CLUB Leseni hii huruhusu uuzaji wa pombe kwa kiasi chochote kwa mwanachama wa Klabu na wageni wao tu
COMBINED 4
Leseni ambazo zimeambatanishwa mhili kwa pamoja:
(a) Combined Hotel and retailers on
(b) Combined Hotel and Restaurant
(c) Combined restaurant and retailers on
TEMPORARY
Leseni hii humruhusu mwenye leseni kuuza pombe katika sehemu iliyotajwa
kwenye leseni mahali penye burudani, starehe au mkusanyiko mwingine kwa
kipindi kisichozidi siku tatu
LOCAL LIQUOR
Class A Local Liquor
Leseni
hii humruhusu mwenye leseni kutengeneza pombe za kienyeji katika sehemu
iliyotajwa na kuuza kwa ajili ya kunywea sehemu ya biashara au nje ya
sehemu ya biashara
Class B Local Liquor
Leseni
hii humruhusu kutengeneza pombe ya kienyeji sehemu iliyotajwa na kwenda
kuuzia sehemu nyingine iliyo na leseni ya kuuza pombe za kienyeji
Class C Local Liquor
Leseni
hii humruhusu kutengeneza pombe ya kienyeji katika sehemu iliyotajwa
kwenye leseni na kuuza kwa mwenye class D au Class E
Class D Local Liquor
Leseni hii humruhusu kuuza pombe za kienyeji katika sehemu iliyotajwa kwenye leseni kwa kunywea eneo la biashara
Class E Local Liquor
Leseni hii humruhusu kuuza pombe za kienyeji kwa ajili ya kunyewea sehemu nyingine mbali ya eneo la biashara
MASHARTI YA KUPATA LESENI
Mtu
yeyote raia wa Tanzania anayo haki ya kupatiwa leseni ya Vileo ili
mradi awe ametimiza umri wa miaka kumi na nane (18) mwenye akili timamu
ambaye hajawahi kupatikana na kosa la jinai na awe na eneo la kufanyia
biashara linalokubalika kisheria.
Kwa mtu ambaye sio raia wa Tanzania anapaswa kuwa na kibali kinachomruhusu kufanya biashara nchini kutoka Idara ya Uhamiaji.
UTARATIBU WA KUPATA LESENI
• Mwombaji hujaza fomu za maombi zinazotolewa na Manispaa
•
Eneo/jingo linalokusudiwa kufanyia biashara hiyo kukaguliwa na Afisa
Afya, Afisa Mipangomiji, Polisi, Afisa Mtendaji wa Kata (WDC) na Afisa
Biashara wa Manispaa na hutoa maoni yao kwenye fomu husika
• Maombi hayo hupelekwa katika Malaka ya Utoaji wa Leseni za Vileo ya Manispaa kwa uamuzi
•
Mwombaji ambaye maombi yake yamepitishwa hupewa Leseni baada ya kulipa
ada inayotakiwa na ni lazima amekamilisha masharti ya kupata leseni hapo
juu
MASHARTI
YA UTUMIAJI Leseni za vileo zina masharti mengi ikiwa ni pamoja na
kutouza kilevi 6 kwa watoto. Masharti mengine ni muda wa kuuza pombe na
kelele za muziki.
MUDA WA KUUZA POMBE BAA (RETAILERS ON)
• Jumatatu hadi Ijumaa - Saa 12.00 jioni hadi saa 5.00 Usiku
•
Jumamosi, Jumapili na Sikukuu - Saa 5.00 asubuhi hadi saa 8.00 mchana
na saa 12.00 jioni hadi saa 6.00 usiku GROSARI (RETAILERS OFF)
• Jumatatu hadi Ijumaa - Saa 2.00 asubuhi hadi saa 1.00 jioni
• Jumamosi, Jumapili na Sikukuu - Saa 3.00 asubuhi hadi saa 6.00 mchana RESTAURANT LICENCE (MGAHAWA)
• Jumatatu hadi Ijumaa - Saa 6.00 mchana hadi saa 8.00 mchana na saa 12.00 jioni hasi saa 6.00 usiku
•
Jumamosi, Jumapili na Sikukuu - Saa 5.00 asubuhi hadi saa 8.00 mchana
na saa 12.00 jioni hadi saa 6.00 usiku MAKOSA Baadhi ya makosa chini ya
sheria hii:
•
Kuruhusu biashara nyingine isiyokubalika kisheria kufanyika eneo la
biashara • Kuuza pombe kwa mtu mwenye umri chini ya miaka kumi na sita
(16)
• Kuajiri mtu chini ya miaka kumi na sita (16) kuuza pombe
• Kuruhusu mtu mwenye umri chini ya miaka kumi na sita kukaa eneo la kuuzia pombe
• Kutoweka leseni sehemu ya wazi, ambapo itaonekana kwa urahisi na wakaguzi
• Kumruhusu/kuleta fujo katika eneo la biashara
• Kuruhusu eneo la biashara kutumika kama danguro
• Kuuza pombe muda ambao ni kinyume cha sheria
• Kufanya biashara ya pombe kwa kutumia leseni ya vileo ambao haistahili
ADHABU
Mfanyabiashara anayetenda mojawapo ya makosa haya akikamatwa,
atafikishwa mahakamani na akitiwa hatiani atalipa faini au kifungo au
adhabu zote kwa pamoja.
UTARATIBU WA USHURU WA MALAZI (HOTEL LEVY) CHINI YA SHERIA NA. 23 YA 1972 MASHARTI YA KULIPIA HOTEL LEVY
1.
Kila mmiliki wa nyumba ya wageni (Guest House) anapaswa kulipa kodi ya
asilimia ishirini (20) ya malipo ya nyumba (Guest House charges) kwa
mwezi husika. Wamiliki wenye mauzo yanayotozwa kodi ya zaidi ya Tshs. 40
milioni kwa mwaka hawatalipa kodi ya malazi bali watalipa Kodi ya
ongezeko la tghamani (VAT)
2. Kodi iliyowekwa, italipwa kuanzia tarehe moja hadi tarehe saba ya mwezi unaofuata mauzo
UTARATIBU WA KULIPIA HOTEL LEVY
•
Malipo ya Ushuru wa Malazi ni lazima yaambatanishwe na fomu ya mapato
ya kila siku (fomu H.L. 1) au kitabu cha wageni, na fomu ya mapato ya
kila mwezi (fomu H.L.2)
•
Mmiliki wa nyumba analeta fomu H.L.1 au kitabu cha wageni pamoja na
fomu H.L. 2 ambaye amekwisha jaza. Afisa anayekadiria atapitia H.L.1 au
kitabu cha wageni na fomu H.L. 2 ili kuhakikisha ni sawa na kuhakikisha
mmiliki amefikia vizuri asilimia 20 ya mapato ya malazi ya mwezi.
•
Mmiliki akishindwa kulipa ushuru kwa muda uliopangwa, siku saba (7)
baada ya mwezi husika kumalizika, atalipa nyongeza ya asilimia 25 ya
ushuru unaotakiwa kulipwa, na endapo ataendelea kutokulipa adhabu
(penalty) itakuwa inaongezeka kwa asilimia kumi (10) ya ushuru
uliotakiwa kulipwa kila baada ya siku thelathini (30) kumalizika MAKOSA
• Mmiliki wa nyumba ya kulala wageni kushindwa kulipa ushuru wa malazi kwa muda unaotakiwa
• Kushindwa au kukataa kuwasilisha fomu ya mapato ya kila mwezi
• Kushindwa kuweka na kutunza kitabu chenye kumbukumbu sahihi za kulala wageni
• Kushindwa kutoa risiti, hati za madai na kumbukumbu nyinginezo kama sheria inavyotaka
• Kumzuia Mkurugenzi au Mwakilishi wa Mkurugenzi katika kufanya kazi zake zilizowekwa na sheria au Kanuni za Ushuru wa Malazi
•
Kushindwa kutekeleza Ilani iliyotolewa na Kamishna/mkurugenzi ya kuitwa
na kuwasilisha nyaraka zinazohusu nyumba yake ya kulala wageni
•
Kutoa taarifa ya uongo kwenye kumbukumbu yeyote inayotumika kwa ajili
ya kudanganya au kushindwa au kukataa kujibu maswali vizuri kwa Afisa wa
Serikali aliyepewa madaraka na sheria hii ADHABU
•
Mmiliki atakayetenda mojawapo ya makosa yaliyotajwa hapo juu atalipa
faini isiyopungua Tshs. 50,000.00 kwa Mkruugenzi wa Manispaa na
isiyozidi Laki tano (500,000.00) Mahakamani akipatikana na hatia.
•
Mmiliki anayekwepa kulipa Ushuru wa Malazi kwa makusudi akikamatwa na
kutiwa hatiani atalipa faini isiyozidi shilingi milioni mbili
(2,000,000.00)
Hata
hivyo kila halmashauri ya wilaya na miji zina utaratibu wake ambao ni
vema mfanyabiashara akachukua hatua katika kufahamu ili kuepuka uvunjaji
wa kanuni za uendeshaji wa biashara na kuepuka adhabu.

No comments:
Post a Comment